Want to partner with us? Let's get started now!

MATUMIZI YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA TANZANIA KATIKA ASASI ZA KIFEDHA

Mikutano ya mwaka ya Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), iliyofanyika mjini Bali Indonesia ambapo imewakutanisha wadau wa masuala ya fedha wakiwemo Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu kutoka nchi mbalimbali Duniani kujadili Sera na misaada inayotolewa na Taasisisi hizo.

Tanzania ni moja ya nchi zilizoshiriki mkutano huo kwa kuwakilishwa na waziri wa fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango. Katika mambo makuu yaliyojailiwa, Benki ya Dunia imeahidi kuwekeza nchini Tanzania katika Sayansi na Teknolojia ili kuongeza kasi ya maendeleo ya kiuchumi kwa lengo la kuisaidia Tanzania kukuza uchumi wa viwanda na kuondoa umasikini kwa wananchi wake.

Benki ya Dunia imeamua kuwekeza katika teknolojia kwa kuwa ni eneo sahihi linaloweza kukuza uchumi wa Taifa kwa zaidi ya mara mbili kutokana na tafiti zilizofanywa na Benki hiyo. Dkt. Mpango amesema kuwa “Kimsingi Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia amefurahia agenda za maendeleo za Tanzania kuhusu kujenga uwezo wa rasilimali watu katika kukuza uchumi wa viwanda na ameahidi kuanza kwa kuwekeza zaidi kwa watoto wenye umri mdogo ili mipango ya maendeleo ya nchi iwe endelevu”

Waziri Mpango pia alimueleza Makamu wa Rais wa Benki hiyo kuwa Tanzania imeweka mikakati mbalimbali ya kujenga uchumi wa viwanda utakaotumia malighafi za ndani ili kuongeza ajira kwa wananchi walio wengi.

Pia Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Bw. Ghanem, ameahidi kuwekeza zaidi katika miradi ya pamoja kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPP), kwa kuiwezesha Serikali ya Tanzania na wadau wengine kwenda kupata mafunzo yatakayoongeza ujuzi wa utekelezaji wa miradi hiyo katika nchi zilizofanya vizuri katika eneo hilo ili kuongeza ufanisi wakati wa utekelezaji wa miradi hiyo.

Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia ameahidi kutembelea Tanzania mwanzoni mwa mwaka ujao ikiwa ni juhudi za kuendeleza ushirikiano wa kimaendeleo kati ya benki hiyo na Tanzania.

Katika kutekeleza mipango endelevu yenye tija, Singo Africa Limited ipo tayari kujumuika na mpango wa Benki ya dunia katika kutoa elimu na uwekezaji wa sayansi na teknolojia ili kuweza kufanikisha sera ya viwanda.

About the Author

Leave a Reply

You may also like these