Wadau mbalimbali wa vyama vya ushirika walioshiriki jukwaa hilo mkoani Kigoma.
Jukwaa la ushirika lililoandaliwa kwa wanaushirika mbalimbali wa vyama vya ushirika wa mkoa wa Kigoma chini ya Ndg. Godfrey Vedasto Rwehumbiza ambaye ni kaimu mrajis msaidizi wa vyama vya ushirika mkoani hapo.
Mkoa huu umebarikiwa kuwa na vyama mbalimbali vinavyojihusisha na ufugaji wa nyuki, wakulima (michikichi, maharage, kahawa na pamba), mafundi seremala, vyama vya akiba na mikopo nk.
Kauli mbiu ya jukaa hili ilikuwa “Ushirika kwa Uzalishaji wa Bidhaa za Viwanda na Nguvu ya Soko”, nae mgeni rasmi katika jukwaa hilo katibu tawala wa wilaya ya Kasulu Mheshimiwa Titus Muguha ameelezea kuwa “Ushirika kama ushirika hauwezi kuwepo kama hakuna kinachozalishwa, na kinachozalishwa ndio bidhaa yenyewe na nguvu ya soko haiwezi kupatikana kama hakuna mikakati yenye hoja na maadhimio dhabiti na sio ya kisiasa”
Kwa upande wake kaimu mrajis wa mkoa wa kigoma Ndg. Godfrey Vedasto Rwehumbiza amesema “ Kutokana na kasi ya ukuaji wa bidhaa na dhana ya ushirika kusimamiwa ipasavyo, yupo tayari kwa kuwa mfano bora wa ushirika wenye manufaa mkoani Kigoma, kwa kufanikisha hilo nitashirikiana na wadau mbalimbali wenye tija katika ushirika. Pamoja na yote uwekezaji kwenye sekta ya teknolojia ndio msingi mkuu wa ushirika mkoani hapa. Hatuwezi kuwa na bidhaa za viwanda , hatuwezi kuwa na nguvu ya soko , hatuwezi kuwa na ushirika na dhana kuu ya ushirika kusimama kama hakutakuwa na taarifa sahihi na takwimu sahihi. Hivyo teknolojia itasaidia kutatua matatizo hayo kwa urahisi.”
Singo Africa Limited ambao ni wadau wakubwa wa ushirika katika sekta ya TEHAMA, waliweza kushiriki maadhamio ya jukwaa hilo kwa kuwa tayari kushirikiana kutoa elimu kwenye vyama ushirika kwa ukaribu kuanzia ngazi za wanachama, viongozi, maafisa ushirika pamoja na wadau wa ushirika mkoani hapo. Pia kwa kushirikiana na Mrajisi msaidizi na vyama vyake, kampuni ya Singo Africa Limited ipo tayari kupanga mikakati na dira ya pamoja katika kukuza ushirika mkoani hapo.
Ushirika kwa pamoja kujenga uchumi wenye nguvu na endelevu zaidi.