Siku ya SACCOS Duniani inayotambulika kama International Credit Union Day (ICUD) inayofanyika kila alhamisi ya tatu(3) ya mwezi wa kumi (10); mwaka huu nchini Tanzania imefanyika katika mkoa wa Iringa viwanja vya Kichangani Kihesa.
Siku hii imehudhuriwa na wana SACCOS mbalimbali nchini ikiongozwa na mgeni rasmi Waziri wa Kilimo nchini Mheshimiwa Charles Tzeba (MB), katika sehemu ya hotuba yake alisema “Swala la ushirika na serikali ya awamu hii ya awamu ya 5 sio la mchezo, wamo ambao hawaamini bado kwamba ushirika utasimama, lakini lazima niwaambieni kwamba ushirika utasimama iwe kwa hiari au kwa lazima” .
Inaaminika aliyasema hayo kutokana na kauli mbiu kuu ya siku hiyo inayosema,
Mafanikio yoyote ili yaitwe mafanikio lazima yapitie kwenye changamoto fulani, hivyo SACCOS zetu nchini zimepitia na zinaendelea kupitia changamoto hizo kama:-
- Ufanisi wa kusimamia mikopo pamoja na dhamana. (Hii ni kukosa nyenzo zinazorahisisha kazi kama tekinolojia za kisasa, mfano TEHAMA)
- Kutokuwa na bidhaa ama huduma stahiki kwa walengwa – TEHAMA inarahisisha hii kazi mno
- Kutokuwa na utawala ulio bora – Utawala bora pamoja na mambo mengine unachagizwa na uwepo wa taarifa sahahi, timilifu na kwa wakati.
- Ushirikiano baina ya SACCOS mbalimbali kuwa hafifu
Siri ya mafanikio makubwa haikwepeki ikiwa vyama vyetu vya akiba na mikopo vikifanya yafuatayo
- Kuimarisha umoja wa SACCOS na namna ya kuongeza ufanisi kwa kwa kupunguza gharama za uendeshaji na usimamizi lakini kuongeza ubora wa huduma kwa wateja.
- Kufanya kazi na wadau mbalimbali wa ushirika kwa karibu ili kuweza kuongeza ufanisi wa mikopo na tija ya mikopo ya chama kwa wanachama wake
- Kuwekeza katika teknolojia sahihi, imara na zenye tija
Singo Africa Limited imechukulia kwa mtizamo chanya sana kauli mbiu ya mwaka huu, na ikiwa ni moja ya washiriki wa siku hiyo, imejipanga vyema katika kuleta mafanikio makubwa katika vyama vya akiba na mikopo. katika hili si uwekezaji wa Teknolojia pekee, bali katika kila hatua ya ushirikiano na vyama hivyo katika kutoa ushauri unaofuata sheria, kanuni na sera za ushirika pamoja na kutoa mafunzo yenye tija ili kuibua SACCOS mpya zenye mafanikio chanya na yenye uendelevu.