Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania – TCDC, iliyo chini ya Wizara ya Kilimo na Ushirikia ikishirikiana na Bank Kuu ya Tanzania -BoT waliandaa mafunzo na mkutano kwa ajili ya watoa huduma katika vyama vya ushirika nchini.
Watoa huduma hao kutoka nyanja mbalimbali kama vile:- TEHAMA (Technology Service Providers), Ukaguzi wa Mahesabu (Auditors), Wakusanya Madeni (Credit Collectors), Wanaotoa Elimu na Mafunzo (Training) Washauri wa Biashara (Consulants), pamoja na wanaotoa huduma za kifedha na Bima-(Microfinance Service Providers).
Mafunzo hayo yalihudhuriwa na Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini Dr. Tito Haule, ambaye alisema kwamba “Kwa uongozi wa sasa wa watoa huduma, nimeona kuna hatua imepigwa na kuona maadili yanafuatwa ukilinganisha na kipindi cha nyuma, uongozi huu umepata Katibu ambaye ni mtaalamu katika ushirika na hivyo kuhamasisha watoa huduma wengine kuona umuhimu wa kupata elimu ya ushirika ili kupata huduma iliyo na vigezo na sheria za ushirika”
Alisistiza kuwa umuhimu wa kwanza na wa haraka kwenye vyama vya ushirika kwa sasa ni kuwekeza katika huduma za kiteknolojia.
Hii itasababisha kuwa na taarifa na takwimu sahihi zenye uwazi na ukweli kwa wana ushirika wote.
Pia watoa huduma hao waliweza kupata elimu mbalimbali ikiwamo ile ya misingi ya ushirika, maadili ya watoa huduma, TEHAMA, sheria za ushirika pamoja na sheria mpya za asasi ndogo za kifedha ya mwaka 2018.
Pamoja na mafunzo hayo Tume ya Maendeleo ya Ushirika imepokea changamoto mbalimbali kutoka kwa wadau wa ushirika na kutoa majibu ya papo kwa papo maana imeonekana changamoto nyingi zimekuwa sugu na kutotatuliwa kwa wakati.
Aidha Mkurugenzi wa Kitengo cha Utafiti na Mafunzo Bi. Doroth Kalikamo, ameweza kutolea ufafanunuzi juu ya changamoto mbalimbali ikiwa na Tume ya Maendeleo ya Ushirika, kuwashirikisha watoa huduma kwenye nyanja mbalimbali za kiuchumi ili kuweza kupanua wigo wa utoaji huduma. Pia ameeleza changamoto nyingi zinatokana na kutokujua sheria na kufanya kwa mawazo yetu na sio utaratibu wa sheria unaotakiwa.
Katibu Mkuu wa watoa huduma nchini Bi. Leah Mbilinyi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara katika kampuni ya Singo Africa Limited amesema “Kushukuru pekee kupata mafunzo haya hakutakuwa na tija yoyote ikiwa hakuna hatua zitakazochuliwa na watoa huduma, ya kujua na kufuata sheria za ushirika ili kuweza kutoa huduma safi na stahiki kwa wateja wetu ambao ni vyama vya ushitika nchini”
Ameongeza pia kwa kusema “Nidhamu na maadili mema yatapatikana pale tu, uwazi utakuwepo baina ya watoa huduma, Tume ya Maendeleo ya Ushirika pamoja na vyama vya ushirika, na hiyo yote lazima uwekezaji wa teknolojia upewe kipao mbele na kuheshimiwa”, ieleweke wazi kwamba kila pale huduma za TEHAMA zilipewa umuhimu ukuaji wa sekta husika ulibadilika, chukulia mfano kwy sekta ya afya maduhuli ya vituo vya afya yalivyopanda kwa asilima zaidi ya mia moja na pending hata mia tano…
Singo Africa Limited ambaye ni mtoa huduma katika sekta ya TEHAMA na pia mshauri wa maswala ya fedha nchini kupia kitendo chake cha Amala App Suite, imekuwa mdau mkuu wa ushirika katika kutoa huduma katika vyama vya ushirika kwa ufanisi na weledi mkubwa na mshirika mzuri katika kushiriki maswala mbalimbali ya ushirika nchini.