Want to partner with us? Let's get started now!

Mafunzo ya TEHAMA katika ushirika mkoani Tanga

Singo Africa Limited waendesha mafunzo ya siku tatu(3) mkoani Tanga juu ya mageuzi na mabadiliko ya TEHAMA katika vyama vya ushirika nchini. tarehe 30/5/2018 mpaka 1/6/2018

Kampuni ya Singo africa Limited kwa kushirikiana na Mrajisi wa vyama vya ushirika mkoa wa Tanga  Jacqline Senzighe, wameendesha mafunzo juu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wakiwashirikisha wadau mbalimbali kutoka SACCOS mbalimbali nchini zikiwemo za Dar es Salaam, Arusha, Kilimanjaro, Mbeya pamoja na Simiyu.

TEHAMA ni kifupi cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, inamaanisha teknolojia za kisasa inayowezesha watu kupata taarifa na mawasiliano kwa kupitia njia ya intaneti, kompyuta, simu na njia nyingine zinazofanana na hizo

Katika ulimwengu wa sasa TEHAMA inazidi kuwa ya muhimu na mataifa mbalimbali yamefanya mapinduzi kwenye nyanja mbalimbali kwa kutumia TEHAMA, na serikali ya Tanzania inatambua umuhimu wa TEHAMA kwenye kuleta maendeleo yake kama kurahisisha njia za utumaji na upokeaji fedha, na kuleta mabaoresho kwenye utoaji huduma katika sekta mbalimbali ikiwemo ya Fedha.

Baadhi ya vyama vya ushirika wa akiba na mikopo vilivyoshiriki mafunzo hayo ni pamoja na, TAZAMA SACCOS, NYUMBA SACCOS, TIRDO SACCOS, PRIME FUEL SACCOS, UWAMU SACCOS, BARIADI TEACHERS SACCOS, HAI TEACHERS SACCOS, UDEA SACCOS, ELCT SACCOS, TANZANIA PASTORS SACCOS, ECLOF SACCOS, DCTW SACCOS, KINONDONI LUTHERN SACCOS pamoja na TRA SACCOS….

Mafunzo hayo yaliambatana na vitendo vya matumizi ya TEHMA na kuleta tija kwa washiriki wa mafunzo hayo na kuwapa uwanja mpana wa kuelezea changamoto mbali mbali za TEHAMA na namna gani zinaweza kutatulika na kuona umuhimu wa matumizi yake.

Nae mrajisi msaidizi wa mkoa wa Tanga, Jacqline alisema haya “Teknolojia ya habari na mawasiliano imekuwa kiungo muhimu sana katika Maendeleo ya watu Duniani.; mfano rahisi ni mitandao ya kijamii

–  Unapata habari/maelezo/taarifa ya bidhaa au huduma kwa haraka zaidi

–  ufanyaji na urahisishaji wa kazi mbalimbali

–  ukusanyaji takwimu kwa urahisi

–  uandaaji wa taarifa” aliendelea “kupitia teknolojia tunataka Vyama vipate faida, vipunguze majanga na matumizi ya rasilimali ili wadau pia wanaotumia/wanaohitaji taarifa zetu ziwe katika ubora na usahihi”

Singo Africa Limited inatoa wito kwa vyama vya ushirika pamoja na taasisi mbalimbali za kifedha kwamba umuhimu wa kiteknolojia haukwepeki na kutokana na mabadiliko yanayotokea kwa sasa hatuwezi kuyakabili pasipokuwa na utumiaji wa kiteknolojia. Kwa kutambua umuhimu huo, kampuni hii inakuletea mifumo rahisi kwa bei nafuu utakaokuwezesha kufanya kazi ya ushirika kwa kufuata taratibu, sheria na kanuni za ushirika na asasi za kifedha, kukuletea matokeo chanya kwa urahisi.

About the Author

Leave a Reply

You may also like these