Singo Africa Limited yashiriki katika jukwaa la vyama vya ushirika mkoa wa Dar es salaam lililo fanyika mnamo tarehe 21/06/2018 hadi 22/06/2018 Police Mercy Ostrerbay, likiwa ni jukwaa la pili toka kuanzishwa kwake mwaka 2016, kama mdau muhimu katika sekta hiyo kwa huduma za mifumo ya TEHAMA na mshauri mtalaamu katika maswala ya matumizi ya TEHAMA kwenye vyama vya ushirika.
Singo Africa Limited ikiwa moja ya wadau wakuu wa ushirika waliweza kupata fursa ya kutoa hotuba fupi na kuwasilisha mada muhimu kwa maendeleo ya Ushirika na Sekta kwa ujumla, walieleza juu ya nguzo muhimu za ushirika na mambo muhimu yapasayo kufanywa na vyama vya ushirika ili kuwepo kwa tija na maendeleo.
Lengo kuu la kuanzishwa kwa jukwaa ni kuwaleta pamoja wadau wa sekta, vyama vya ushirika vikubwa na vidogo wajifunze, wabadilishane uzoefu na kuibua changamoto zinazokabili sekta ya ushirika, kuainisha fursa zilizopo na pia kuweka mikakati ya kutatua changamoto kwa kutumia fursa zilizopo. Naye mrajisi wa vyama vya ushirika alieleza juu ya uzingatiaji sheria(compliance) na kuvitaka vyama viache kuenenda pasipo kuzingatia misingi waliyokubaliana katika kuvisimamia vyama na kuviendeleza.
Singo Africa Limited kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kama Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini, Chuo kikuu cha Ushirika Moshi, Shirika la ukaguzi wa hesabu za vyama vya ushirika, taasisi mbalimbali za fedha na mifuko mbalimbali ya jamii imekubali kwa moyo mmoja kushirikiana na hao wadau ili kuweza kuvipeleka mbele vyama vyetu vya ushirika kwa kuwekeza katika teknolojia endelevu yenye tija ili kuvisaidia vyama vya ushirika katika kurahisisha na kuleta ufanisi kwenye kazi zao.
Nae Mwakilishi kutoka Singo Africa Limited Bi. Joyce Isaya alisema “Ikiwa Ushirika ni msingi wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii, itakuwa ngumu kupata hayo maendeleo ikiwa bado tunafanya shughuli zetu kwa hali ya kimazoea (business as usual), itambulike kuwa tunaitaji kubadilika, na kufuata taratibu, kanuni na sheria zinazotuongoza katika misingi ya kimaendeleo ili kukuza sekta na vyama kwa ujumla.
Uchumu na Maendeleo yoyote ya ushirika hayaji kwa urahisi pasipo gharama, hivyo ni muda sahihi kwa Mkoa wa Dar es salaam na Tanzania kwa ujumla kubadilisha mawazo hasi katika teknolojia na kuweka mawazo chanya ili kuinua vyama vyetu vya ushirika katika ngazi zote.