Mkoa wa Tanga kwa kushirikiana na wanaushirika wote umekuwa na mwitikio chanya katika maswala ya Ushirika, hivyo mrajisi msaidizi wa vyama vya ushirika mkoani Tanga Jacquline Senzige kwa kushirikiana na wadau mbalimbali aliandaa jukwaa hilo tarehe 26/06/2018 katika ukumbi wa Mkuu wa mkoa. Singo Africa Limited ikiwa moja ya wadau wakuu waushirika waliweza kupata fursa ya kualikwa na kuwa washiriki wakuu katika jukwaa hilo.
Lengo kuu la jukwaa hilo ni kukutanisha wadau wa ushirika wa mkoa na kushirikishana pamoja ili kubadilishana uzoefu, kuibua changamoto zinazokabili sekta ya ushirika, kuainisha fursa zilizopo na pia kuweka mikakati ya kutatua changamoto kwa kutumia fursa zilizopo.
Singo Africa Limited kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kama Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini, Chuo kikuu cha Ushirika Moshi, Shirika la ukaguzi wa hesabu za vyama vya ushirika, taasisi mbalimbali za fedha na mifuko mbalimbali ya jamii imekubali kwa moyo mmoja kushirikiana na hao wadau ili kuweza kuvipeleka mbele vyama vyetu vya ushirika kwa kuwekeza katika teknolojia endelevu yenyetija ili kuvisaidia vyama vya ushirika katika kurahisisha kazi za wadau.
Nae Mkurugenzi wa maendeleo ya biashara katika ushirika Singo Africa Limited Leah Mbilinyi amesema ” Ikiwa Ushirika ni msingi wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii, itakuwa ngumu kuleta hayo maendeleo ikiwa bado tunafanya shughuli zetu kwa hali ya kimazoea(business as usual), itambulike kuwa tunaitaji kubadilika, na mageuzi sahihi kwa sasa ni kukubaliana na mabadiliko ya kiteknilojia,hivyo, ili kujenga uchumi unahitajika uwekezaji wa hali ya juu wa teknolojia na ulio sahihi. Ni Singo Africa Limited pekee ambayo imeuelewa ushirika katika teknolojia na ipo tayari kufanya mageuzi kwa maendeleo chanya ya uchumi wa ushirika.”. Aliongeza, na kutoa wito kwa wadau na vyama vya ushirika katika kutumia mifumo ya kitechnologia yenye tija na manufaa itakayochochea maendeleo chanya kwenye vyama na ushirika kwa ujumla.
Maendeleo yoyote hayaji kwa urahisi pasipo maumivu na gharama, hivyo ni muda sahihi kwa Mkoa wa Tanga na Tanzania kwa ujumla kubadilisha mawazo hasi ya kiteknolojia na kuweka mawazo chanya ili kuinua vyama vyetu vya ushirika katika ngazi zote.