Want to partner with us? Let's get started now!

Siku ya Ushirika Duniani – Mwanza

Kongamano la Kitaifa la Wanaushirika limefanyika  Julai 06, 2018 ikiwa ni siku moja kabla ya Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani ambayo huazimishwa kila mwaka ifikapo Jumamosi ya kwanza ya mwezi Julai.

Siku ya Ushirika Duniani kwa mwaka huu imefanyika Julai 07, 2018 Jijini Mwanza katika viwanja vya Furahisha ambapo Kauli mbiu yake ni “Ushirika kwa Ulaji na Uzalishaji Endelevu wa Bidhaa na Huduma.”

Nae mgeni maalumu katika kongamano la maandalizi ya siku ya Ushirika duniani, Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt. Charles Tizeba, amewataka viongozi na Wasimamizi wa vyama vya Ushirika kuzibaini changamoto mbalimbali zinazoikabili Sekta ya Ushirika na kuzitatua ili vyama vya ushirika viwe imara na vyenye tija kwa wanachama na wananchi kwa ujumla.


Akifungua Kongamano la Kitaifa la Wanaushirika lililofanyika katika viwanja vya Furahisha Jijini Mwanza, Dkt. Tizeba amesema kuwa Tanzania inabidi kujitafakari na kuweza kujua sababu zinazopelekea watu wasijiunge na vyama vya ushirika.
“Watanzania tupo milioni 54, lakini Wanaushirika wa vyama vyote ni chiniya asilimia 10 ya Watanzania wote, sasa tuanzie hapo katika kutafakari kitugani kimetokea watu hawajiungi tena katika ushirika” alisema Waziri Tizeba.

Siku ya maadhimisho hayo, mgeni rasmi alikuwa ni Waziri mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa, akiongelea kuhusu kauli mbiu ya mwaka huu hakuacha kusema kwamba ushirika umeimarishwa kwa mabadiliko yanayotokea kwa kipindi hiki 

“Vyama vya ushirika nchini vimeanza kuimarika ikilinganishwa na miaka iliyopita, kuwataka viongozi wenye dhamana  kuendelea kusimamia vyama hivyo ili vilete tija kwa wananchi.”

Pia amesema kuimarika kwa vyama hivyo kunatokana na mabadiliko yaliyofanywa na Serikali ya kuweka mfumo na utaratibu wa kuendesha ushirika.

“Viongozi wenye dhamana endeleeni kusimamia vyama hivi ili kuleta tija kwa wakulima, imefikia hatua wananchi waliondoa imani kwa sababu ya utendaji mbovu wa viongozi wasio waadilifu,” amesema.

Kuhusu soko huria, amesema halina tija kwa wakulima baada ya kutokea watu wanaowarubuni na kuuza mazao yao kwa misingi ya kuwapa fedha za haraka lakini kwa gharama ndogo.

Amesema serikali haiwezi kuacha ushirika ukaendeshwa kienyeji, “tunataka tuwe na watu wenye ueledi. Vyama vya msingi ndio vyenye dhamana ya kuhakikisha mazao ya wakulima yananunuliwa na kupata haki zao badala ya vyama vikuu vya ushirika kusimamia jambo hilo.”

Singo Africa Limited ambao ni wadau wakuu wa ushirika katika sekta ya TEHAMA, iliweza kuudhuria na kushiriki siku hiyo na kupata nafasi ya kuongea na  wadau wa ushirika kwamba mabadliko ya ushirika yanavutia na yanakwenda kwa kasi lakini Teknolojia ikikwepeka basi mabadiliko hayo yatafika mahali yatakwama na kushindwa kuendelea, nae mkurugenzi wa maendeleo katika kampuni ya Singo Africa Limited Bi. Leah Mbilinyi akiongea kwenye hafla fupi baada ya maadhimisho alisema ” Tafakari kuu inayosababisha watu wasijiunge na ushirika itaondolewa pale tu imani ya misingi ya ushirika itakaporudi kwa uwazi, na uwazi huo hauwezi kuonekana kama tutabaki bila mabadiliko ya kuwekeza katika teknolojia, lakini pia pamoja na uwekeaji huo lazima elimu ya mabadiliko ipokelewe kwa mikono miwili na viongozi wakubali maumivu ya mabadiliko ikiwa ni pamoja na kuingia gharama ya uwekezaji wa teknolojia” 

Singo Africa Limited ni Kampuni pekee ya kiteknolojia iliyoudhuria siku hiyo na kupata nafasi ya kukutana na wanaushirika mbalimbali na kuchukua hatua ya kufanya mabadiliko kwa vyama hivyo kutokana na changamoto na matatizo wanayowakabili wanaushirika.

About the Author

One thought on “Siku ya Ushirika Duniani – Mwanza

Leave a Reply

You may also like these