Want to partner with us? Let's get started now!

USIMAMIZI WA MIKOPO KATIKA ASASI ZA KIFEDHA

Bidhaa kubwa ya asasi  za kifedha ni biashara ya fedha. Biashara ya fedha ni mbadilishano wa fedha na fedha, na mbadilishano huo wa kifedha unatumika kama kukopeshana.

Hivyo basi tutambue kwamba mkopo ni kiasi cha fedha, mali na bidhaa ambazo mtu/chama/taasisi kimetoa kwa mwanachama na hatimaye kurudisha katika muda fulani uliokubalika pamoja na riba.

Anaechukua mkopo atambue kwamba ile pesa au mali aliyochukua si mali yake, inamilikiwa na mtu/taasisi fulani.

Usimamizi wa mikopo umekuwa ni changamoto kubwa kwenye asasi za kifedha kutokana na ukosefu wa elimu kwa wakopeshwaji, pia taasisi fulani kushindwa kubuni mikopo ambayo inaweza kusimamiwa kwa umakini kuweza kuwa na takwimu sahihi na  zenye tija kwenye taasisi.

Kuna vitu muhimu vya kutambua katika sekta hii muhimu ya mikopo kwenye asasi zetu za kifedha ili kuweza kuimarisha usimamizi wa mikopo kwenye taasisi zetu

  • Je tuna mikataba sahihi ya huduma kwa wateja wetu?
  • Je tunawatambua wateja wetu ipasavyo?
  • Je tuna elimu ya kutosha katika shughuli za mikopo na kutambua taasisi zetu?
  • Je bodi / kamati na kitengo cha mikopo kinatambua wajibu wake?
  • Je mikataba yetu ya mikopo ipo katika hali ya kisheria?
  • Tuna pata nafasi kubwa ya kutambua mikopo chechefu na athari zake?
  • Ni rahisi kwa taasisi zetu kuchambua na kutoa riport sahihi za mikopo yetu?

Kutokana na mikopo kuwa ndio bidhaa mama za taasisi zetu, inashauriwa kwamba uwekezaji wa mifumo sahihi na rahisi ni njia pekee ya kuweza kuleta takwimu sahihi za mikopo yetu, lakini si takwimu pekee bali kuweza kusimamisha taasisi na kuwa na umakini katika kazi kuu ya usimamizi wa mikopo.

Singo Africa Limited ni kampuni ya kiteknolojia  na ushauri wa kitaalamu; katika ushauri jukumu kuu ni kuwekeza katika teknolojia ambayo ni rahisi kusimamia mikopo kuanzia kumtambua mteja, anavyokopa, ni nani aliyehusika kuruhusu mkopo huo utoke, pia atakavyokuwa anarejesha na kutoa taarifa iliyokamili katika mikopo. Hivyo basi ubunifu wa bidhaa mbalimbali haitazuia katika ukuaji wa taasisi bali itaborasha kwa kuleta taarifa zilizo sahihi na kuleta sifa njema kwa taasisi zetu.

Kwa minajili hiyo, usimamizi wa mikopo katika taasisi zetu utaboreshwa na kuwa makini zaidi katika uwekezaji wa kiteknolojia ulioidhinishwa na wadau sahihi wa kifedha nchini.

About the Author

Leave a Reply

You may also like these