Siku ya wakulima [8 8] Tanzania kila mwaka inaadhimishwa tarehe nane [8] ya mwezi wa nane [8] , Mwaka huu Tanzania ikiwa ni maonyesho ya 25 (Ishirini na tano) , kauli mbiu ya mwaka huu ni “Wekeza katika KILIMO, MIFUGO na UVUVI kwa maendeleo ya VIWANDA”
Singo Africa Limited moja ya kampuni inayojishughulisha na sekta ya viwanda na ushirika kwa ujumla iliweza kushiriki katika kanda ya mashariki iliyofanyika mkoani Morogoro katika viwanja vya Julius Kambarage Nyerere.
Lengo kuu ni kuweza kufahamu changamoto na nini wanaona ni njia rahisi ya kuweza kuwekeza katika kilimo, mifugo, uvuvi ili kuweza kuleta maendeleo ya viwanda.
Bi. Leah ambaye ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara na Mtaalamu Mshauri wa Ushirika na Microfinance wa kampuni ya Singo Africa Limited iliweza kuonana na sekta mbali mbali , iliweza kukutana na Mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania (MVIWATA) “Taasisi hii ni ya watanzania wote ambao ni wakulima, ni chombo kinachosimama kwa ajili ya wakulima, ina vikundi mbalimbali na taasisi mbalimbali za kifedha. Kuna malengo mbalimbali pamoja na shughuli za kiushirika kuanzia ngazi ya kijiji mpaka kitaifa ila inahudumiwa kwa njia za vikundi.
Changamoto kubwa ni kuweza kupata wadau wa maendeleo hasa kwenye sekta ya takwimu sahihi; na wanaamini njia pekee ni kuwekeza katika teknolojia” aliyasema haya Bw. Joseph Sengasenga mwezeshaji wa kiuchumi mkoa.
Pia aliweza kuwashukuru kampuni ya Singo Africa Limited kutembelea banda lao na kuweza kujua changamoto mbali mbali zinazopatikana katika sekta hii ya kilimo hasa kilimo biashara na uendeshaji wa vikundi katika levo mbalimbali.
Singo Africa Limited, ipo tayari kushirikiana na wakulima wote katika mnyororo wa thamani ili kuweza kuleta matokeo yaliyo chanya katika sekta nzima ya kilimo na kuweza kuka na vikundi mbalimbali kwenye mnyororo huo ili kuweza kufahamu changamoto mbalimbali na kuzitatua kwa namna ile ambayo ni sahihi.
Thanks for sharing. I read many of your blog posts, cool, your blog is very good. https://accounts.binance.com/ka-GE/register-person?ref=DB40ITMB