Amala Times

Singo Africa Limited yashiriki katika jukwaa la vyama vya ushirika mkoa wa Dar es salaam lililo fanyika mnamo tarehe 21/06/2018 hadi 22/06/2018 Police Mercy Ostrerbay, likiwa ni jukwaa la pili toka kuanzishwa kwake mwaka 2016, kama mdau muhimu katika sekta hiyo kwa huduma za mifumo ya TEHAMA na mshauri mtalaamu katika maswala ya matumizi ya TEHAMA kwenye vyama vya ushirika.

Kongamano la Kitaifa la Wanaushirika limefanyika  Julai 06, 2018 ikiwa ni siku moja kabla ya Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani ambayo huazimishwa kila mwaka ifikapo Jumamosi ya kwanza ya mwezi Julai.

Siku ya Ushirika Duniani kwa mwaka huu imefanyika Julai 07, 2018 Jijini Mwanza katika viwanja vya Furahisha ambapo Kauli mbiu yake ni "Ushirika kwa Ulaji na Uzalishaji Endelevu wa Bidhaa na Huduma."

Mkoa wa Tanga kwa kushirikiana na wanaushirika wote umekuwa na mwitikio chanya katika maswala ya Ushirika, hivyo mrajisi msaidizi  wa vyama vya ushirika mkoani Tanga Jacquline Senzige kwa kushirikiana na wadau mbalimbali aliandaa jukwaa hilo tarehe 26/06/2018 katika ukumbi wa Mkuu wa mkoa.

Singo Africa Limited waendesha mafunzo ya siku tatu(3) mkoani Tanga juu ya mageuzi na mabadiliko ya TEHAMA katika vyama vya ushirika nchini. tarehe 30/5/2018 mpaka 1/6/2018

Kampuni ya Singo africa Limited kwa kushirikiana na Mrajisi wa vyama vya ushirika mkoa wa Tanga  Jacqline Senzighe, wameendesha mafunzo juu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wakiwashirikisha wadau mbalimbali kutoka SACCOS mbalimbali nchini zikiwemo za Dar es Salaam, Arusha, Kilimanjaro, Mbeya pamoja na Simiyu.

Page 14 of 18

About us

A technology for financial inclusion that has features for financial institution flexibility to grow and advance in its way of managing customers, financial products, fast and regular reporting capabilities.

Powered by Mifos  

Lets Grow Together

 

Service Desk[existing clients only]

 
Contact us

SingoAfrica Limited
Mbezi Beach "B"  | Mwai Kibaki Road | 6 Wasafi Str.

P.O BOX 78908 | 14121 Dar es Salaam

This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. | +255 71 262 8896 | singo.africa | amala.co.tz

Newsletter

Please subscribe to our Newsletters to always stay updated.
Top